Aliyekuwa Naibu Rais Nchini, Rigathi Gachagua amedai kuwa hayuko salama na kubainisha kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kumuua kwa kumuwekea sumu kwenye chakula mara mbili.
Alipokuwa akizungumza na wanahabari akiwa anatoka hospitalini Karen alipolazwa wakati alipougua akipokea matibabu, Gachagua anaelezea kuwa, ” Ruto hakuwa na nia ya kufanya kazi na mimi”, alitaka tuu kunitumia kupata uungwaji mkono ili aweze kushinda uchanguzi,”
” Kwa ya kwanza, niseme ilikuwa mnamo Agosti tarehe 30, huko mjini Kisumu kwangu, ambapo walinzi wa siri waliingia chumbani kwangu kwa nguvu na mmoja wao alidhubutu kunitilia sumu kwenye chakula, lakini tuligundua na tukaweza kuepuka na mpango huo,” Gachagua alikiri hayo.
“Na mnamo Septemba huko Nyeri, timu nyingine ilikuja na kujaribu kunitilia sumu kwenye chakula ambacho kilikusudiwa kuwa changu na Baraza la wazee wa kikuyu”
Rigathi Gachagua aliendelea kumshutumu Rais Ruto na lalama zake dhidi yake na kudai kuwa amesaliti makubaliano waliokuwa nayo kabla ya kuingia Mamlakani mwaka wa Elfu mbili na ishirini na mbili.
Aliyekuwa Naibu wa Rais huyo pia aliendelea kwa kusema, “Ruto atawajibika iwapo lolote litanitendekea” alisema Gachagua huku akiongeza kuwa ilimbidii awaondoe baadhi ya maafisa wa ujasusi katika afisi Lake kwa kuwa walikosa kuaminika.