KENYA KUCHUANA NA TANZANIA KATIKA FAINALI LA KUSAKA UBINGWA WA CECAFA KWA WACHEZAJI WASIOZIDI UMRI WA 20

Timu ya taifa ya soka ya Kenya chini ya umri wa miaka 20 imefuzu michuano ya AFCON 2025.

Kenya imejikatia tiketi ya kushiriki Michuano hiyo mikubwa baada ya kuifunga Burundi “Intamba Murugamba” mabao 4-0. Huku mabao ya Kenya yakifungwa na Lawrence okoth, Hassan Beja, Aldrin Kibet na Luis Ingavi.

Mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam leo.

Kwa upande mwingine, Tanzania ilifuzu kushiriki AFCON mwaka ujao baada ya kuwalaza Uganda mabao 2-1.

Time zote mbili sasa zitachuana katika finali la kusaka ubingwa wa CECAFA u20 Mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *