ARTETA, ATETEMESHWA PAMOJA NA WANAWE WABUNDUKI.

Ligi kuu ya soka ya Uingereza iliendelea tena hapo jana Oktoba 19, 2024. Kwa mchezo wa kukata na shoka kati ya wenyeji Bournemouth na wageni wao Arsenali. Ambapo wenyeji waliweza kuibuka na ushindi baada ya kuwalaza mabao 2-0. Mabao ya Bournemouth yaliweza kutiwa kimyani na R. Christie katika dakika 70, huku J.Kluivert alizidisha bao pili kupitia mkwajo wa penalti katika dakika la 79, Kwa sasa kulingana na msimamo wa ligi hio wanabunduki wamo katika nafasi ya tatu. Huku wakiwa wamejizolea alama kumi na saba baada ya kuingia ugani mara nane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *